Header Ads

Harmorapa asema kua show za mikoani na biashara za nje ya nchi zimempunguzia kiki

Msanii muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) aliyekuja kwa kasi na kupotea- Harmorapa amedai hajaishiwa kiki kama wengi wanavyodai.Harmorapa ameeleza kuwa ukimya wake unasababishwa na biashara anazofanya nje ya muziki pamoja na show zake za mikoani ambazo amekuwa akifanya mara nyingi.
“Nipo bize sana na mishe nyingine nje ya muziki, namaanisha mimi ni mfanyabiashara, so huwa mara nyingi nasafiri, mara nyingi huwa napiga tour zangu mikoani na project zangu za muziki zipo kama kawaida” amesema.
Ameongeza kuwa kutokana na hilo ni vigumu sana kumkuta Dar es Salaam kwani anakuwa bize sana.

No comments