Header Ads

Gigy Money aongelea ishu ya kupata mtoto

Msanii wa muziki na video queen Bongo, Gigy Money amesema mwakani anatarajia kupata mtoto.

Gigy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Papa’ ameiambia E Fm Radio kuwa hicho ni kitu ambacho yeye na mpenzi wake wameshakaa na kukijadili.
“Watengemee tu mwakani nitakuwa na mtoto Mungu akinisaidia, yaani hiyo ni lazima” amesema Gigy Money.
Katika hatua nyingine Gigy Money ameongeza kuwa huu ni mwaka wa tatu yupo na mpenzi wake hivyo ni muda sahihi kufanya hivyo.

No comments