Zaidi ya 1500 wahamishwa kwasababu ya volkano kulipuka Papua New Guinea

Karibu watu 1,500 wamehamishwa kutoka visiwa vya Papua New Guinea, ambapo mlima ambao umekuwa umetulia kwa muda mrefu ulianza kulipuka, kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.
Volkano katika kisiwa cha Kodovar ilianza kutoa moshi na majivu wiki iliyopita, na kusababisha kuhamishwa kwa zaidi ya watu 500 kwenda kisiwa kilicho karibu cha Blup Blup.
Baada ya mlipuko kuzidi sasa wale waliokimbilia kisiwa cha Kodovar sasa watahamishiwa kwingine.
Papua New Guinea ni nyumbani kwa milima kadhaa ya volkano.
- Hatari kubwa ya mlipuko wa volkano Bali
- Hatari kwa ndege baada ya Volkano Bali
- Hofu ya kulipuka volkano katika kisiwa cha kitalii cha Bali
Walioshuhudia huko Blup Blup kusini mwa kisiwa cha Kadovar waliripoti mlipuko mkubwa kutoka kwa volkano siku ya Ijumaa na moto mkubwa ukitoka kwenye mlima huo.
Wanasayansi baadaye waligundua viwango vikubwa vya gesi ya sulphur dioxide kutoka na volkano hiyo.

Post a Comment