Utafiti: Jeraha la mchana hupona haraka kuliko lile la usiku

Wanasayansi nchini Uingereza wamegundua kwamba majeraha ya kukatwa na kuchomeka hupona haraka yanapopatikana mchana ikilinganishwa usiku.
Wanasema kwamba ni kutokana na mwili unavyohisi kulingana na muda.
Utafiti huo unasema kuwa seli za ngozi ya mwanadamu hubadilisha tabia yake kulingana na muda huku protini zinazohitajika kurekebisha majeraha hayo zikifanya kazi vizuri wakati wa mchana.
Jeraha la kuchomeka nyakati za usiku lilichukua siku 28 kupona ikilinganishwa na siku 17 za jereha la wakati wa mchana.
Watafiti walitaja tofauti hiyo kuwa kubwa huku wakiongezea kwamba wanaweza kuharakisha watu kupona kwa kutumia dawa za steroids ambazo hubadilisha muda wa mwili.
Post a Comment