Hizi ndizo Mechi 13 za Taifa Stars chini ya Salum Mayanga tangu March 2017

Stars inaingia kwenye mchezo huo chini ya Mayanga ikiwa imecheza mechi 13, imeshinda michezo 6, sare 6 huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu. Katika mechi hizo Stars imefunga jumla ya magoli 15 na kuruhusu kufunga magoli 9 na kufanya wastani wa magoli kuwa 6.
Mechi 13 ambazo kocha Salum Mayanga ameiongoza Stars tangu alipokabidhiwa juku hilo kutoka kwa Charles Boniface Mkwasa
Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)- Tanzania 2-1 Burundi (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
- Tanzania 1-1 Lesotho (kufuzu AFCON)
- Tanzania 2-0 Malawi (COSAFA)
- Angola 0-0 Tanzania (COSAFA)
- Tanzania 1-1 Mauritius (COSAFA)
- Afrika Kusini 0-1 Tanzania (COSAFA)
- Zambia 4-2 Tanzania (COSAFA)
- Tanzania 0-0 Lesotho (Stars ilishinda kwa penati 4-2 COSAFA)
- Tanzania 1-1 Rwanda (kufuzu CHAN)
- Rwanda 0-0 Tanzania (kufuzu CHAN)
- Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
- Tanzania 1-1 Malawi
Post a Comment