BURUDANI Chin Bees ameeleza sababu za kupewa mkataba na Management mpya

April 11 2017 kupitia kipindi cha Sizi Kitaa kinachoruka kupitia Clouds TV staa wa rap Chin Bees amezungumzia sababu za kuzingatia kwa msanii pindi anapopata mkataba na management mpya.
Akiulizwa swali kuhusu uwezo wake aliounesha hadi kupelekea kupewa mkataba naWanene Entertainment, Chin Bees amesema kitu cha kuzingatia ni kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa umeingia makubaliano.
>>>”Kikubwa ni kuzingatia kupiga kazi maana unaposaini mkataba na mtu unakuwa kama umeajiriwa, so kuna kazi inabidi uifanye. Hata yule unayefanya naye kazi aone kuna kitu cha kuongeza. Tumeachia wimbo wangu wa Pepeta, watu wameupenda kwa sababu una-sound kinyamwezi na kinyumbani pia hadi nchi za nje. Hiyo ni kutokana tunapiga kazi.” – Chin Bees.
Post a Comment